Mkurugenzi Ofisi ya Rais Anaswa kwa UTAPELI, Muroto Afunguka – Video

Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Girres Muroto.

JESHI  la Polisi mkoani Dodoma linamshikilia Simon Saulo Ngatunga 38 aliyekuwa Mkurungenzi wa Utumishi katika Wizara ya Ofisi ya Rais Tamisemi – Sikonge, Tabora,  na mfanyabiashara mmoja kwa tuhuma za utapeli.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Girres Muroto wakati akizungumza na wanahabri jijini humo.

Tumemkamata mtu mmoja anaitwa Hassan Katundu (29) mfanyabiashara na mkazi wa Yombo-Buza jijini Dar es Salaam, alikuwa akijifanya ofisa usalama wa taifa, na kuwatapeli wananchi akiwalaghai wampatie pesa ili awatafutie nafasi za kazi.  Baada ya kutimuliwa kazi, aliyekuwa Mkurugenzi wa Utumishi Ofisi ya Rais Tamisemi Sikonge, Simon Ngatunga, amekuwa akimtumia huyu ofisa feki wa usalama wa taifa kumtafutia ajira, hivyo wote tumewatia mbaroni na upelelezi ukikamilika tutawafikisha mahakamani.

Katika tukio la pili, tumemkamata Didiona Julius mkazi wa Dar es Salaam ambaye anamiliki Kampuni ya VGKP ambayo inajishuhulisha na kupima viwanja, huyu  amekuwa akijidai kuwa anauza viwanja, anachukua pesa anatokomea nazo; amewatapeli wananchi wa Dar, Arusha, Dodoma na mikoa mingine, na amekuwa akisababisha migororo ya ardhi na kesi nyingi za wananchi zimefika kwa Waziri wa Ardhi, William Lukuvi.  Huyu amekamatwa pamoja na mkewe, na atapelekwa Dar es Salaam.

Katika tukio la tatu, tumemkamata Salum Salim (31), mkazi wa Tabata Shule ambaye amekuwa akijifanya ofisa wa mfuko wa hifadhi wa PSSF. Anawalaghai wastaafu anashughulikia mafao yao, anawadanganya mafaili yao yapo mezani kwake hivyo wampe pesa ayashughulikie ili walipwe pesa zao. 

Aidha, Muroto amesema Jeshi hilo linaendelea na msako kwa matapeli wote mkoani humo huku akitoa rai watafute sehemu nyingine wala si Dodoma kwani hakuna nafasi na watakamatwa tu. Pia, amewataka madereva wanaoendesha vyombo wazingatie sheria za barabarani kuepuka ajali, mwendokasi, kuchukua tahadhari wenye mabasi na wasipandishe nauli kiholela na wenye magari mabovu yasiingie barabarani.

Toa comment