The House of Favourite Newspapers

Mkurugenzi wa Global awapongeza wanaye kuhitimu kidato cha nne

0

Baba wa Catherine akimkabidhi zawadi mwanaye.

Catherine akimlisha keki baba yake, Masha Bukumbi, kwenye hafla hiyo. 

Catherine (kulia) akijiandaa kumlisha keki  baba yake.

Agnes Manyilizu  akimlisha keki babake mdogo,Masha,  kwenye hafla hiyo.

Catherine (kulia) akimlisha keki  dadake, Salah Masha Bukumbi.

Mama  wa Agnes Manyilizu aitwaye Monica Manyilizu,  akilishwa keki na mwanaye kwenye hafla hiyo.

Catherine (kulia) alimlisha keki mdogo ake aitwaye James Bukumbi.

Mama wa Catherine, Alice Masha,  akilishwa keki iliyokuwa imeandaliwa.

Mama wa Catherine akiwa katika picha ya pamoja.

Agnes (kushoto) na Catherine wakiwa katika picha ya pamoja huku wakishikilia keki zao.

Mwonekano wa keki  za Agnes Manyilizu na Catherine.

Baadhi ya wanafamilia wakiwa katika picha ya furaha.

Mkurugenzi wa Global Publishers Ltd, Masha Bukumbi (aliyeshikilia cheti) akiwa katika picha ya pamoja na wanafamilia wake.

MKURUGENZI wa Global Publishers Ltd, Masha Bukumbi, amewapongeza wanaye wawili, Catherine Masha Bukumbi na mtoto wa kaka yake, Agnes Manyilizu kwa kuhitimu kidato cha nne.

Masha aliwapongeza wanaye hao jana katika hafla ya mahafali ya kumaliza kidato cha nne kwenye Shule ya Sekondari Ujenzi iliyopo Wilaya ya Mkuranga-Pwani ambako alikuwa amehudhuria akiambatana na familia yake na ya Paschal Manyilizu.

Akizungumza na wanaye hao, Masha alisema kuwa anawatakia mtihani mwema kuelekea kipindi chao cha kufanya mtihani wanaotarajia kuufamya Novemba pili mwaka huu, akisema ni wajibu wao kwa muda uliobaki wasome kwa bidii ili sherehe hiyo iweze kusindikizwa kwa kufaulu mitihani yao.

Aliwasisitiza kuwa mafaniko yao hayatakuja pasipo kujituma kwa kusoma kwa bidii na kushirikiana na walimu wao kwa kutenda mema yenye kuendana na sheria na taratibu za shule, pasipo kumsahua Mungu.

“Mafanikio yenu hayataonekana pasipo kujituma, kushirikiana na walimu wenu kwa kuwa na mapenzi mema kwao hivyo sasa hafla hii ya leo isindikizwe kwa kufaulu mitihani yenu,” alisema Masha.

NA DENIS MTIMA/GPL-Mkuranga

Leave A Reply