Mkurugenzi wa Shirika la Ndege ATCL Ahukumiwa Jela

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka alipofika leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kutolewa hukumu.

 

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mataka na mwenzake Elisaph Mathew, aliyekuwa Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha cha ATCL kwenda jela miaka sita kila mmoja au kulipa faini ya jumla ya Sh. Milioni 70 (Milioni 35 kila mmoja).

 

Mbali na adhabu hiyo, mahakama pia imewaamuru watuhumiwa hao kulipa hasara waliyoisababishia ATCL katika ununuzi wa magari chakavu 26 ambayo ni dola za Marekani 143,442.75 sawa na Sh. Milioni 322.

Aidha mahakama hiyo imemuachia huru William Haji ambaye aliyekuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Ndani za ATCL.

 

Mattaka alipandishwa kizimbani mara ya kwanza mwaka 2008 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akituhumiwa kwa matumizi mabaya ya ofisi kwa kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. bilioni moja zilizotumika kununua magari machakavu.

Breaking News: Jambazi Aliyeongoza Mauaji ya Polisi 8 Kibiti Auawa -Dar


Tuhuma hizo ni pamoja na kusaini mkataba wa kukodisha ndege aina ya Air Bus A320-214 kwa Kampuni ya Wallis TradingInc bila kufuata sheria na taratibu za zabuni. Alidaiwa kuiingizia hasara serikali kutokana na hatua yake ya kuidhinisha pesa za matengenezo ya ndege hiyo katika Kampuni ya AEROMANTENIMIENTO.

Hasara nyingine zilikuwa ni matumizi mabaya kwa kununua vifaa vya ndani ya ndege hiyo yaliyoigharimu Dola za Marekani 35,984.82.

NA DENIS MTIMA | GPL

Wolper Amemtukana Harmonize Matusi ya Nguoni?


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Loading...

Toa comment