The House of Favourite Newspapers

Mkuu wa Chuo cha Mwanafunzi Aliyepigwa Risasi Afunguka (Video)

Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji NIT, Zakaria Mganilwa ameeleza masikitiko yake baada ya kupokea taarifa rasmi ya kifo cha mwanafunzi wao, Aquilina Akwilini aliyepigwa risasi na kufariki jana February 16, 2018 wakati polisi wakizuia maandamano ya wafuasi wa CHADEMA katika eneo la Mkwajuni.

 

Akizunumza na Global TV Online mchana wa leo, Mganilwa amesema baada ya kupokea taarifa hizo, chuo kiliwatuma mwakilishi wa Bodi ya Usimamizi wa Chuo, Mwangalizi wa Wanafunzi, pamoja na mwakilishi mwingine wa Serikali ya Wanafunzi katika chuo hicho kwenda katika Hospitali ya Mwananyamala ili kutambua mwili wa marehemu na baada ya kutambua ni yeye, wamewasiliana na familia ya marehemu ambao wanaishi Mbezi ya Kimara kwa ajili ya mipango ya msiba huo.

VIdeo: Msikie hapa akizungumza.

Comments are closed.