Mtanzania Mbaroni Kwa kuiibia Serikali ya Marekani Bilioni 8!

MTANZANIA JOHN NDUNGURU, anayemiliki kampuni ya Mercy Services of Heath inayojishughulisha na kazi ya  kuhudumia wagonjwa majumbani (Home Health Care) nchini Marekani, ametiwa mbaroni nchini humo na kufunguliwa mashitaka 12 ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Kwa mujibu wa mtandao wa NBCWASHINGTON.COM, ulioandika habari hiyo Desemba 3 mwaka huu, Ndunguru anadaiwa kujipatia kiasi cha dola za Marekani milioni 3.6 (T.shs Bilioni 8) baada ya kuandika nyaraka za madai ya uongo akionesha kuidai serikali ya jimbo la Virginia kiasi hicho akionesha kampuni yake kuhudumia wagonjwa wapatao 59.

Tukio hilo limetokea wakati Jimbo la Virginia linajitayarisha kupanua mpango wa msaada wa tiba na hati za mahakama zinaonyesha kwamba idara inayoshughulikia huduma za tiba tayari imelipa Dola mil. 3.6 kwa kampuni ya Ndunguru.

Trina Greene, ambaye ni meneja katika kampuni hiyo, alisema wafanyakazi walishtushwa na habari hizo, lakini bado wako bega kwa bega na mkuu wao ambaye humwita Dr. John.

Green na wafanyakazi wengine walianza kuhisi dadlili za matatizo wiki iliyopita wakati ofisi yao ilipovamiwa na wapelelezi kutoka ofisi ya mwanasheria mkuu ambapo kompyuta 10 zilichukuliwa pamoja na masanduku 33 ya hati mbalimbali.

Hati za mahakama zinadai kwamba kulikuwa na saini ya daktari mmoja iliyoghushiwa na rekodi za watu kadhaa waliopata huduma hapo hazionekani zilipo.

Kampuni hiyo hutoa huduma kwa watu wapatao 90 na imeajiri wafanyakazi wapatao 100.

Ndunguru yuko rumande nchini Marekani baada ya kukosa dhamana.

Toa comment