Mkuu wa Majeshi, Jenerali Mkunda Akutana na Mkuu wa Usalama wa Jeshi la India
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob John Mkunda amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Usalama wa Jeshi la India, Luteni Jenerali Dokta Dinesh Singh Rana ofisini kwake, Upanga jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao, Jenerali Mkunda amesema kuwa ujio wake ni ishara ya kudumisha mahusiano kati ya Tanzania na India hasa katika nyanja za kidiplomasia ya kijeshi, mafunzo, kubadilishana uzoefu wa kijeshi na taarifa za kiusalama.
Mkuu wa Usalama wa Jeshi la India amefika ofisini kwa Jenerali Mkunda kumsalimia ikiwa ni sehemu ya ziara yake hapa nchini.
Wakati huo huo, Jenerali Mkunda amekutana na Mwambata Jeshi wa Jeshi la Malawi nchini Tanzania, Kanali Orion Msukwa alipofika ofisini kwake Upanga jijini Dar es Salaam kuaga baada ya muda wake wa kuliwakilisha Jeshi la Malawi hapa nchini kuisha.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu – JWTZ