IKIWA ni saa chache baada ya Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde kutangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha nne wa 2017, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Marian Girls iliyopo Bagamoyo mkoani Pwani ambao wameshika nafasi ya sita Kitaifa, Lightness Masawe amefunguka mengi kuhusu ufaulu huo.
Akizungumza na Global Publishers, Madam Masawe amesema anamshukuru Mungu kwa ushindi huo mzuri ulioziletea heshima shule zao zote za Marian Girls na Marianm Boys.
Marian Girls imekuwa shule ya sita Kitaifa na kutoa mwanafunzi bora wa pili, wa tatu na wa tisa Kitaifa huku Marian Boys ikishika nafasi ya tisa Kitaifa na kutoa mwanafunzi Bora wa kwanza Kitaifa.
“Wanafunzi wetu tunawalea katika maadili mazuri, wanajituma kwa bidii na wanawasikiliza vyema walimu wao darasani. Kutokana na misingi yetu ya dini, watoto wetu wanakuwa watiifu na wasikivu hivyo ni rahisi kwao kutekeleza mambo yote wanayoelekezwa na walimu wao kwa ajili ya manufaa yao,” alisema Madam Masawe.
Orodha ya Shule 10 Bora.
1. St. Francis Girls – Mbeya
2. Feza Boys – Dar es Salaam
3. Kemoboya – Kagera
4. Bethel Sabs Girls – Iringa
5. Anwarite Girls – Kilimanjaro
6. Marian Girls – Pwani
7. Canossa – Dar
8. Feza Girls – Dar
9. Marian Boys – Pwani
10. Shamsiye Boys – Dar
Comments are closed.