Mkuu wa Mkoa Dar afungua semina ya mafuta na gesi

3Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, James P. Mataragio, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Meck Said na Kelvin Komba.
4Baadhi ya wanahabari wakifuatilia semina hiyo iliyokuwa ikiendelea katika Ukumbi wa Mikutano Karim Jee Dar.2. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Mecky Said (katikati) pembeni yake ni wafanyakazi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wakiwa katika picha ya pamoja. Waliopo nyuma yake ni waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Mecky Said amefungua Semina ya Mafuta na Gesi jijini Dar es Salaam ikiwahusisha waandishi wa habari wa vyomba mbalimbali hapa nchini.

Mkuu huyo wa mkoa amefungua semina hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Karim Jee jijini Dar es Salaam ambapo pia washiriki walipata fursa ya kupiga picha ya pamoja na kiongozi huyo.

Akizungumza katika semina hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), James P. Mataragio, amesema kuwa lengo kubwa la semina hiyo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu uelewa wa sekta ndogo ya mafuta na gesi.

Amesema semina hiyo itaweza kuwajengea waandishi wa habari ujuzi wa kuandika habari nzuri na zenye kutoa elimu miongoni mwa wananchi kufahamu namna ya uzalishaji na uchakataji wa gesi asilia na hivyo kupitia semina hiyo kuwa na manufaa zaidi.

(Na Denis Mtima/GPL)


Loading...

Toa comment