The House of Favourite Newspapers

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Apokea Msaada Kutoka NMB

0
Wakionesha fulana zilizotolewa na NMB.

Katika kuunga mkono jitihada za uthibiti wa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini, leo ikiwa Siku ya Ukimwi
duniani, Benki ya NMB imetoa msaada wa ticheti zilizovaliwa katika hafla ya maadhimisho mjini Moshi na elimu
kuhusu umuhimu wa kukata bima ya afya.

 

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Anna Elisha Mghwira amepoka msaada huo uliotolewa na benki ya NMB kwa ajili ya maadhimisho hayo ya siku ya  ya Ukimwi duniani.

Meneja wa NMB Tawi la Nelson Mandela, PrayGod Godwin akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira Msaada wa Tisheti zilizovaliwa katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniania leo ofisini kwake. 
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko(kushoto) akizungumza na Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro (Kati), Meneja wa NMB Tawi la Nelson Mandela, PrayGod Godwin na  Meneja Mwandamizi Huduma za Serikali, Christabel Hiza mara baada ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani iliyofanyika mjini Moshi, mkoa wa Kilimanjaro.
Mgeni rasmi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Stella Msofe akipata maelezo kutoka kwa Meneja Mahusiano Biashara na Serikali wa Benki ya NMB, Mkunde Joseph alipotembelea Banda la Benki hiyo kwenye maadhimisho yaliyofanyika katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es Salaam leo. 
Leave A Reply