The House of Favourite Newspapers

MKUU WA MKOA WA TANGA AFIKA KUMZIKA MAJUTO (PICHA +VIDEO)

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,  Martin Shigela,  akiwa nyumbani kwa marehemu Amri Athumani ‘Mzee Majuto’ jijini Tanga.

MWILI  wa aliyekuwa msanii gwiji wa filamu nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’,  unatarajiwa kuzikwa leo mkoani Tanga katika shamba lake lililopo katika kijiji cha Kiruku ambako maeneo ya Donge ambako viongozi mbalimbali wa serikali,  akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela, wamefika kushiriki maziko yake.

 

Mzee Majuto alifariki usiku wa Jumatano, Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Muhimbili, ambapo kesho yake, Agosti 9, 2018 mwili wake ulipelekwa katika Msikiti wa Maamur, Upanga, jijini Dar es Salaam, kuswaliwa kabla ya kupelekwa viwanja vya ukumbi wa Karimjee kuagwa. Baadaye mwili huo ulisafirishwa kuelekea jijini Tanga kwa maziko.

Marehemu ameacha mjane na watoto kumi.

Innah Lillah Wainna Ilaih Rajiun.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela akisalimia  waombolezaji.
Umati wa waombolezaji.

(PICHA: RICHARD BUKOS/ GPL -TANGA)

Comments are closed.