Mkuu wa Shule atoboa Siri ya Ufaulu matokeo ya kidato cha sita, Nidhamu Na Ushirikiano Nyenzo Ya Matokeo Mazuri
Nidhamu kwa wanafunzi ,ufundishaji mzuri unaofanywa na walimu wa shule hiyo ndiyo sababu pekee iliyofanya shule hiyo kupata matokeo mazuri kwenye matokeo ya kidato cha sita mwaka 2024.
Mkuu wa shule Sekondari Nyampulukano Mathias Misungwi
Mkuu wa hiyo Mathias Misungwi amesema ushirikiano wa wazazi na walimu wamechangia matokeo haya kuwa mazuri na shule yetu kuonekana bora Kwa matokeo ya kidato cha sita mwaka huu shule ya Nyampulukano imefuta daraja la nne na daraja sifuri kama mwaka 2023 huku ikiongeza ufaulu kwa waliopata daraja la kwanza kwa asilimia 11, waliopata daraja pili kwa asimilia 6 na waliopata daraja la tatu kwa asilimia Tano
Matokeo ya waliofanya mtihani wa kidato cha sita daraja kwanza 182 daraja la pili 115 na daraja tatu 6 mkuu wanafunzi watatu kati hawa wamepata daraja la kwanza la pointi tatu jambo ambalo lilikuwa halijawahi kutokea kwenye shule hiyo.
Shule ya Sekondari Nyampulukano, Sengerema – Mwanza
Misungwi ameahidi kupiga hatua zaidi kwenye mitahani ijayo ya kidato cha pili na nne kuongeza ufaulu kwa kufuta daraja la tatu na nne sufulu na kubaki na daraja la kwanza na daraja la pili pekee.
“Nawashukuru walimu wangu wanaosimamia taalumu na nidhamu wamesaidia sehemu kubwa la ufaulu wa wanafunzi huku akipongeza walimu wote kwa kujitoa kuhakikisha shule hiyo inafanya vizuri.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema Binuru Shekidele amesema usimamizi mzuru wa taaluma katika shule zetu ndiyo siri ya mafaniko na Matokeo mazuri ya watoto wetu.
Ametoa wito kwa walimu kuendelea kufundisha kwa bidiii ili kuwasaidia watoto wetu waweze kufika malengo yao.
Pia amepongeza Serikali ya awamu ya sita ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule zetu ambao umechangia wanafunzi kupata mahari salama pa kujifunzi, Baadhi ya wananchi Wilayani Sengerema wamemwagia sifa mkuu wa shule ya Sekondari Nyampulukano Mathias Misungwi Kwa kusimamia vema shule na kupata matokeo mazuri.
Huku wakipongeza utendaji wa mkuu wa wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga ambaye amekuwa bega kwa Baga kuhakikisha wilaya ya Sengerema inachanja Mbuga kwenye sekta zote ikiwemo sekta ya elimu.