Mkuu wa Shule Kisimiri Apewa Tuzo na Global Radio, Apokelewa Kishujaa (Picha +Video)

Mkuu wa Shule iliyoongoza kitaifa katika matokeo ya Kidato cha Sita, Kisimiri High School, Valentine Mathias Tarimo (katikati) na Mwalimu wa Taaluma, Eliutheo Mwanyika (nyuma ya Tarimo)  wakipokelewa na Meneja Mkuu wa Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho (wa pili  kushoto)  akiwa na Mhariri Kiongozi wa Global Publishers, Saleh Ally (kushoto) na Meneja wa +255 Global Radio, Bori Mbaraka (wa tatu kushoto) Julai 17, 2019 katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

MKUU wa Shule ya Sekondari Kisimiri Arusha, Valentino Tarimo,  Jumatano Julai 17, 2019 amekabidhiwa Tuzo ya Shukrani baada ya shule yake kuibuka kidedea kwa kufaulisha na kuwa ya kwanza nchini katika matokeo ya Kidato cha Sita mwaka huu.

Abdallah Mrisho (kulia) akimkabidhi Tuzo ya Shukrani Mwalimu Valentino Mathias.

Mwalimu Tarimo amekabidhiwa Tuzo ya Shukrani na Meneja Mkuu wa Global Group, Abdallah Mrisho kwa niaba ya Global Radio leo baada ya kupokelewa kishujaa na wafanyakazi wa kampuni ya Global Group alipofika ofisini kwao kufuatia mwaliko aliopewa na uongozi wa kampuni hiyo.

Meneja Mrisho alimsifu Tarimo na timu yake kwa kuwafanya wanafunzi hao kuongoza katika ufaulu kitaifa na kuifanya shule yao kuwa ya kwanza.

Meneja wa +255 Global Radio, Bori Mbaraka (kulia) akimkabidhi tuzo ya shukrani  Mwalimu wa Taaluma, Eliutheo Mwanyika

Mwalimu huyo aliyealikwa jijini Dar es Salaam na kituo cha redio ya mtandaoni inayokuja kasi nchini ya +255 Global Radio,  alishukuru familia ya Global kwa kutambua kazi wanayoifanya ya kuelimisha wanafunzi.

Matokeo ya shule hii, yamefungua ukurasa mpya na kuzibeba shule za kata za serikali ambazo kwa muda mrefu zimekuwa hazionyeshi kufanya vizuri.

Kwa mujibu wa  Tarimo, walimu wanaofundisha shule hiyo ni kawaida kwao kufanya vizuri katika kufaulisha.

Katika ziara hiyo Tarimo alifuatana na Mwalimu wa Taaluma, Eliutheo Severine  na mwanafunzi wa kiume aliyefanya vizuri katika masomo ya sayansi, Herman Kamugisha.

Katika matokeo ya mtihani yaliyotangazwa hivi karibuni na Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Taifa, Dk. Charles Msonde, licha ya shule hiyo kuongoza kwa matokeo mazuri, bado hayajakata kiu ya Mkuu wa Shule Mwalimu Tarimo na walimu wenzake kufanya vizuri zaidi.

Stori na Elvan Stambuli


 

Mwalimu Tarimo akisalimiana na wafanyakazi wa Global Group.

 

 

…Akizidi kumiminiwa pongezi. 

…Akisaini kitabu cha wageni.

…Akikabidhiwa gazeti na Mhariri wa Gazeti la Championi Jumamosi, Lucy Mgina (kushoto).

…Akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Global TV Online, Abdallah Ng’anzi.

…Akimsikiliza Ng’anzi aliyekuwa akitoa maelezo katika  studio ya Global TV Online.

Picha ya ukumbusho.


Loading...

Toa comment