MKUU SHULE YA KISIMIRI ATAJA MBINU ZA KUFANYA VIZURI 2019 (PICHA +VIDEO)

Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisimiri Arusha, Valentino Tarimo,  akifanya mahojiano na +255 Global Radio leo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

GLOBAL RADIO leo wamefanya mahojiano na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisimiri Arusha, Valentino Tarimo,  baada ya shule yake kuibuka kidedea kwa kufaulisha na kuwa ya kwanza nchini katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu.

Tarimo amesema shule yake mkoani  wa Arusha ambayo ni ya kata ilianzishwa mwaka 2012, ilipofika mwaka 2016 wakapokea wanafunzi wa kidato cha tano na mwaka 2019 matokeo ya kidato cha sita walikuwa wa pili kitaifa.

”Mwaka 2010 tulitoka kwenye kumi bora tukaenda 12 kitaifa, mwaka 2011 pia tulitoka kumi bora tukawa wa 19 kitaifa mpaka mwaka 2013 hadi leo tupo kwenye kumi bora, na sasa tupo kwenye kumi bora kwa miaka mitatu mfululizo.

”Baada ya serikali kuja na mkakati wa shule ya kata, wapo watu wengi walizibeza shule hizi sana na kuziita majina mengi ambayo siwezi kuyataja hapa mbele ya redio. Tumeonyesha tofauti, tumeonyesha kwa vitendo.

Mtangazaji wa Global Radio na Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul, akifanya mahojiano na Tarimo (hayuko pichani).

”La kwanza Watanzania wajue kuwa shule ni ya serikali, ni shule ya kata na wanafunzi wote kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha tano tunapangiwa na serikali. Wakifika kwetu kazi yetu ni kuwafundisha kwa malengo’.

”Shule yoyote ikijiwekea mipango inaweza kuwa ya kwanza na inaweza kupata matokeo yoyote inayohitaji.  Sisi Kisimiri tuna malengo,  mikakati na utekelezaji wake lazima uwe na usimamizi makini wa malengo.

Mkuu wa GlobalTV Online, Abdallah Ngazi, akifanya mahojiano  na Tarimo  (hayupo pichani).

”Utaona ukiwa na malengo na mikakati na usimamizi wa malengo, sisi kuwa wa kwanza hayakuwa malengo yetu, malengo yetu yalikuwa wanafunzi 60 kupata daraja la kwanza lakini matokeo yalipotoka, wanafunzi 58 wamepata division one na wawili division 2 kidato cha sita mwaka huu.

”Kwa sasa wanafunzi wetu kidato cha kwanza mpaka cha nne wanatoka Kata ya Uwilo, lakini zamani tulikuwa Kata ya Ngarenanyuki lakini hapa kati iligawanywa Kata tatu; Uwilo, Angabobo, na Ngarenanyuki’.

Meneja wa Redio wa Global Radio, Bori Mbaraka (kushoto) akiongea jambo na Tarimo na ujumbe aliofuatana nao. 

”Siku za nyuma tulikuwa hatufanyi vizuri kwa maana form four yetu ya kwanza ilianza 2005 tukapata matokeo yasiyoridhisha 2012, aambapo tulipata zero 145, tukaja na mkakati wa Kisimiri Sawazisha.

”Ilikuwa ikisemekana ukanda wa Kisimiri Juu wanalima  bangi, lakini niwahakikishie waandishi wa habari na Watanzania baada ya serikali ya awamu ya tano, Kisimiri Juu hakuna bangi, lakini wakati wanasema hivyo, shule yetu haijawahi kuwa na kesi ya kuvuta bangi.

Wakati wa kuaagana baada ya kipindi.

”Suala la nidhamu kwetu ni la kwanza, huwezi kupanga kufanya vizuri kitaaluma wakati wanafunzi hawana nidhamu, huwezi kufanikiwa, ukakaa darasani ukawafundisha wavuta bangi.

Kwa habari zaidi za mahojiano hayo, fungua video hapo juu.


Loading...

Toa comment