The House of Favourite Newspapers
gunners X

Mkuu wa Wilaya avamia Gesti

0

Stori:  Salum Yassin, IJUMAA
DAR ES SALAAM:Kasi ya Magufuli! Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam, Ally Hapi Salum (pichani) amevamia gesti moja iliyopo Manzese Tip Top jijini Dar baada ya mwananchi mmoja kumpa malalamiko ya kuwepo kwa akina dada wanaojiuza ‘machangudoa’ na vibaka, Ijumaa liko bega kwa bega.
Tukio hilo la aina yake lilijiri juzi kwenye gesti hiyo iliyopo ndani ya baa maarufu ya Lambo ambapo mkuu huyo wa wilaya alikuwa katika kamatakamata ya wafanyabiashara wanaodaiwa kuficha sukari maeneo ya Manzese zoezi ambalo pia liko nchi nzima.

mkuu wa wilaya kinondoni (8)

Ni wakati DC huyo akipita maeneo hayo na jopo la wasaidizi wake, wakiwemo polisi, mwananchi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Daudi Charles, alimsimamisha na kumpa malalamiko kwamba, Baa ya Lambo inakiuka maagizo ya serikali ya kufunga saa sita usiku kwani yenyewe inakesha.

mkuu wa wilaya kinondoni (6)

“Mheshimiwa mkuu wa wilaya, naomba tusaidie. Hii Baa ya Lambo haifuati maagizo ya serikali, inafanya kazi mpaka kunakucha wakati serikali inataka baa zifungwe saa sita usiku.

mkuu wa wilaya kinondoni (7)

“Halafu kule ndani kuna machangudoa wanajiuza na vibaka wanaibia watu kwa kuwakaba na kutoboa madirisha, yaani ni kero tupu hapa mtaani kwetu, vibaka walishawahi kutoboa dirisha la mama yangu, tusaidie mheshimiwa,” alisema Daudi kwa sauti ya unyenyekevu.

mkuu wa wilaya kinondoni (9)Pia, Daudi aliendelea kusema kuwa, baadhi ya watu wamekuwa wakifanya ngono kwenye vichochoro vya mitaa hiyo kiasi kwamba, watoto wanapopita asubuhi kwenda mashuleni hukumbana na ‘zana’ zilizotumika hali ambayo ni hatari kiafya.

mkuu wa wilaya kinondoni (10)Baada ya kusikia malalamiko hayo, bila kufanya ajizi, mkuu wa wilaya aligeuza mwelekeo na kuingia kwenye baa hiyo na kufanya ukaguzi huku akitaka kujua waliko machangudoa hao huku akitembelea vyumba na kuangalia mazingira kwa ujumla, vikiwemo vyoo na sehemu ya kutolea maji machafu.

mkuu wa wilaya kinondoni (11)

Ndani ya baa hiyo hawakukutwa wahudumu, meneja wala mmiliki zaidi ya mtu mmoja aliyesema yeye kazi yake ni kufanya usafi tu.

mkuu wa wilaya kinondoni (3)

Hata hivyo, mkuu wa wilaya huyo hakutaka kuingia kwenye vyumba vinavyodaiwa kuwa ndiyo gesti licha ya kuoneshwa milango.

mkuu wa wilaya kinondoni (4)

Mwishowe, kiongozi huyo alitoa agizo kwa mkuu wa Kituo Kidogo cha Polisi Tip Top (jina halikupatikana mara moja) kuimarisha ulinzi shirikishi na kufanya oparesheni ili kuwaondoa vibaka na machangudoa.

Kwa kauli hiyo ya mkuu wa wilaya, Daudi alisema yeye binafsi anaunga mkono juhudi hizo kwa kujitolea kuhakikisha ulinzi unaimarika katika eneo hilo ili wakazi wake waishi kwa amani.

 

Leave A Reply