Mkwasa Abwaga Manyanga Ruvu Shooting

 

KOCHA Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ amechana na Klabu ya Ruvu Shooting ya Pwani. Mkwasa ametaja sababu ya kuachana na timu hiyo ni matokeo mabovu.

 

“Nimeamua kuwajibika kutokana na kutotimiza malengo ya klabu. Tumepitia changamoto nyingi hivyo nimeona ni vyema kuacha ili wengine waendelee pale nilipoishia,” amesema Mkwasa.

 

Kufuatia uamuzi huo wa Mkwasa timu hiyo itaongozwa na Kocha Msaidizi, Rajab Nakuchema wakati uongozi ukiendelea kusaka kocha mkuu kuchukua nafasi hiyo.706
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment