The House of Favourite Newspapers

Mlacha Ajishindia Mil. 5 ya Magift ya Kugift Wengine Waondoka na Milioni Milioni

Kampuni ya mtandao wa Mawasiliano ya YAS Tanzania, ikishirikiana na kitengo cha Mixx by Yas ,Leo hii Feb 3  2025, imekabidhi zawadi  kwa washindi 4 wa Shindano la “Magift ya kugift” kwenye Droo ya wiki ya 12  ambapo kati ya hao mmoja akijishindia mil 1.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Meneja wa Bidhaa  kutoka Kampuni ya Yas, Bi Marry Rutha, amewapongeza washindi hao huku akiwataka Watanzania  wengine kuendelea kutumia huduma za kampuni yao kwani huenda wakaibuka washindi.

Rutha amesema mpaka sasa wameshatoa zawadi za fedha zenye thamani ya  kiasi cha  TSh milion 550, kwa washindi wa makundi  tofauti ikiwemo,mawakala,na wateja wengine.

Kwa upande wake mshindi wa wiki hii WA mil 5, Kelvin Joseph  Mlacha akiwakilisha wenziwe 3 waliojinyakulia  mil 1 kila mmoja “amemshukuru Yas kwa  kuchezesha kampeni hiyo ya “MAGIFT ya KUGIFT 2025” na hatimaye yeye kuibuka mshindi, na amewaomba watanzania kushiriki kampeni zinazoletwa na Yas Tanzania kwani hakuna ubabaisha kila mtu anashinda kutokana na Bahati yake amesema Mlacha.Kampuni ya YAS imekuwa na muendelezo mzuri wa kuendesha kampeni mbalimbali ikiwa sehemu ya kujitangaza itakumbukwa kuwa kampuni ya YAS ilizinduliwa hivi karibuni ikichuka pahala la Tigo ambayo imedumu kwa kipindi cha miaka 30 ikitoa huduma zake hapa nchini, na kutunukiwa Tuzo mbali mbali ndani na Nje ya nchi, ikiwemo Tuzo ya mtandao wenye kasi zaidi Barani Africa inayotolewa na OOKLA.

Hii ni wiki ya 12 kati ya wiki 13  ambazo Yas kupitia kitengo cha Mixx by Yas  imeendelea kutoa zawadi Zaidi kupitia kampeni Yao ya “Magift ya kugift” kwa wateja wao kwa msimu wa mwaka 2024-25.Aidha Rutha amesema mpaka sasa wameshatoa zawadi za fedha zenye thamani ya  kiasi cha  TSh milion 550 kwa washindi wa makundi  tofauti ikiwemo,mawakala,na wateja wengine.

Kwa upande wake mshindi wa wiki hii akiwakilisha wenziwe Mary Maros Iseke  ambaye amejinyakulia kiasi cha Shilingi mil 1  “ameishukuru Yas kwa  kuchezesha kampeni hiyo ya “MAGIFT ya KUGIFT 2025” na hatimaye yeye kuibuka mshindi, na amewaomba watanzania kushiriki kampeni zinazoletwa na Yas Tanzania kwani hakuna ubabaisha kila mtu anashinda kutokana na BAHATI yake amesema Marry.

Kampuni ya Yas imekuwa na muendelezo mzuri wa kuendesha kampeni mbalimbali ikiwa sehemu ya kujitangaza Zaidi kwa wateja wake.

Hii ni droo ya wiki ya 12  mfulululizo kati kati ya wiki 13 ambazo Yas kupitia msimu huu wa siku kuu, ikishirikiana na kitengo cha Mixx by Yas,  imeendelea kutoa zawadi zaidi kupitia kampeni yao ya “Magift ya kugift” kwa wateja wao kwa mwaka huu wa 2025.