The House of Favourite Newspapers

Mlinzi wa Mahakama Atuhumiwa Kubaka Mwanafunzi Mahakamani

0

JESHI la Polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia Joseph Masanja (58) mlinzi wa mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Shinyanga kwa tuhuma ya kumbaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 10 wakati akiwa kwenye eneo lake la kazi.

 

Tukio hilo lilitokea Machi 21, 2020, ambapo mtuhumiwa alimdanganya binti huyo aliyekuwa na mwanzake mwenye umri wa miaka saba kwenda katika eneo lake la kazi kwa madai ya kuwapatia fedha za kununua ndala.

 

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi Mkoa wa Shinyanga ACP, Debora Magiligimba, mtuhumiwa alikamatwa baada ya binti hiyo kutoka katika eneo la kazi majira ya saa kumi na moja jioni.

 

“Ilikuwa saa nane mchana siku ya Jumamosi, mabinti hao walifika mahakamani, Joseph aliagiza binti wa miaka saba kubakia getini na kisha yeye kuingia ndani na binti huyu na kumbaka katika moja ya vyumba vya ofisi katika eneo la mahakahama,” alisema Magiligimba.

 

Alifafanua kuwa baada ya kutekeleza tukio hilo Masanja alimwamuru binti huyo kuondoka eneo la tukio kwa kupitia geti lingine ambapo mwalimu mmoja wa Shule ya Msingi Mwenge aliyefamika kwa jina mmoja la Leticia alimkamata binti huyo na kumhoji kuwa ametokea wapi ndipo alipokiri alikuwa akifanya mapenzi na mlinzi huyo.

 

“Kuna afisa wa polisi alimwona binti wa miaka saba aliyekaa getini muda mrefu, alipomhoji kwa nini amekaa kwa muda mrefu katika eneo hilo alijibiwa kuwa anamsubiri mwenzake tangu majira ya saa nane mchana alipoingia ndani na mlinzi huyo hajatoka,”aliongeza Magiligimba.

 

Aliendelea kusema kuwa askari huyo alimchukua binti huyo na kuingia naye ndani ya eneo la mahakama na kukutana na mwalimu aliyemkamata binti yule wa miaka kumi wakati akipitishwa geti la pili na Joseph ndipo walipoamua kutoa taarifa kwa wazazi wa mabinti hao.

 

Aidha alisema kuwa baada ya mabinti hao kufikishwa polisi wazazi wao walifika na kupewa kibali cha kwenda hospitali kwa ajili ya vipimo ambapo  vilibaini kuwa binti huyo alikuwa ameingiliwa (kubakwa).

 

Hata hivyo,  Magiligimba alisema baada ya Joseph kutekeleza tukio hilo alikimbia kusikojulikana hadi alipokamatwa na polisi na alipohojiwa alikiri kumbaka mwanafunzi huyo.

 

Upepelezi wa tukio utakapokamilika atafikishwa mahakani kujibu tuhuma hizo.

Leave A Reply