The House of Favourite Newspapers

Mlinzi wa Rayvanny Apigwa Roba Mbeya

0

MMOJA walinzi wa wasanii wa Bongo Fleva, Rayvanny amejikuta katika wakati mgumu baada ya kunyukwa roba ya mbao na shabiki kule Mbeya.

 

Bado haijulikani ilikuwaje mpaka akapigwa roba, yani mtu unalipwa ili kumlinda bosi wako, harafu unakabwa wewe kwanza kabla ya bosi wako, hii ni aibu kubwa, maana yake kazi huwezi.

 

Tukio hili la kushangaza limeyokea wakati Rayvanny alipojiri mkoani humo kwa ajili ya kutumbuiza siku ya Ukimwi Duniani, Desemba 1, 2021.

 

Ingawa mpaka sasa Rayvanny hajafunguka kilichotokea licha ya kuposti picha na kuonesha kushangazwa na watu wa Mbeya kutokana na kitendo hicho, lakini hii inaonesha jinsi gani walinzi wake walivyo rojorojo.

 

Kwa kawaida mlinzi unatakiwa uwe imara na sio hafifu, ujue majukumu yako na uyatimize vizuri, hivi niulize, huyu mlinzi kama vile wana ugonjwa wa kifaduro au unyafuzi, hivi angekuwa Muddy Mnyama wa Harmonize wangesogea kweli hawa watu wa Mbeya?

 

Rayvanny tambua kwamba wewe ni brand kubwa hivyo unatakiwa uwe na ulinzi wa maana, sio ulinzi rojorojo, kuna siku litatokea jambo watashindwa kuhimili na yatakuwa mjanja.

Leave A Reply