The House of Favourite Newspapers

Mlinzi wa ‘Soja’ Mstaafu Aacha Bunduki Kitandani, Awafungulia Wahalifu

0
Rais Magufuli akimjulia hali Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyelazwa hospitalini Lugalo.

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limetoa taarifa kuhusu tukio la Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata aliyevamiwa na watu wasiojulikana kisha kumpiga risasi juzi Jumatatu, nyumbani kwake eneo la Tegeta Masaiti jijini Dar.

“Taarifa hiyo iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro  Mambosasa alipokuwa akizungumza na wanahabari imeeleza kuwa siku ya tukio, Jenerali Mribata alikuwa amekwenda Benki ya NBC, Tangi Bovu, na baada ya kufanya muamala watu wawili ambao hakuwatambua walimfuatilia kwa pikipiki mpaka nyumbani kwake alipopiga honi ili afunguliwe.

“Kwa maelezo ya mlinzi wa nyumba hiyo ambaye ni askari wa Suma JKT tulipomhoji alisema aliiweka silaha juu ya kitanda kisha kwenda mikono mitupu kufungua geti, ambapo wahalifu waliingia na kutekeleza tukio hilo.

“Baadaye analezea kuwa aliamriwa akimbie, naye akatii, akakimbia bila shuruti akaacha silaha pale. Hakupigwa hata kwenzi, aliondoka akamuacha Meja Jenerali akishambuliwa lakini aadaye alirudi.

“Kwa askari aliyepitia mafunzo ya JKT kama yule hatutegemei kama angeweza kufanya vile, hivyo tuna mashaka naye, mpaka sasa tunamshikilia.

“Tumekwenda eneo la tukio tukabaini kuna mfanyakazi wa benki alikuwa akiwasiliana na wahalifu akiwaunganisha watekeleze uhalifu huo. Huyo naye tumemkamata,” alisema Mambosasa.

Meja Jenerali Mstaafu Vincent Mribata anaendelea kutibiwa katika Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo, Jijini Dar es Salaam kutokana na shambulio hilo.

SHUHUDIA VIDEO YA TUKIO HILO

Leave A Reply