The House of Favourite Newspapers

Mlipuko waua 28 na kujeruhi 61 Uturuki

0

mlipuko 3

Vikosi vya zimamoto vikipambana na moto uliosababishwa na mlipuko.

Smoke from a fire billow is seen following an explosion as police officers secure the area in Ankara, Wednesday, Feb. 17, 2016. A large explosion, believed to have been caused by a bomb, injured several people in the Turkish capital on Wednesday, according to media reports. (Cihan News Agency via AP)

Moshi mkubwa ukitoka katika eneo ulipotokea mlipuko jana mjini Ankara, Uturuki huku wanausalama nao wakiwa eneo hilo.

WATU zaidi ya 28 wamepoteza maisha huku 61 wakijeruhiwa baada ya mlipuko mkubwa kutokea katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara jana jioni, maofisa wa Uturuki wameeleza.

Gari lililojaa vilipuzi lililipuliwa na kuchoma mabasi ya jeshi yalipokuwa yakipita, kwa mujibu wa Ofisi ya Gavana wa Ankara.

mlipuko

Mlipuko huo ulitokea karibu na Bunge na Makao Makuu ya Jeshi la Uturuki.
Naibu Waziri Mkuu, Bekir Bozdag amesema hicho ni “kitendo cha ugaidi”.

Moshi ulitanda angani kutoka eneo hilo na watu walioshuhudia tukio hilo wanasema mlipuko huo ulisikika kote katika mji huo.

Baadhi ya waliofariki na kujeruhiwa walikuwa raia na mpaka sasa hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulio hilo.

Credit: BBC

Leave A Reply