The House of Favourite Newspapers

LOWASSA ATOA KAULI KWA TAIFA STARS NA TFF

WAZIRI Mkuu wa zamani Edward Lowassa amewataka wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kucheza kama Morani wa Kimasai katika mechi yao ya marejeano dhidi ya Cape Verde katika  Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, leo Jumanne, Oktoba 16, 2018.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, amewataka wachezaji hao wa Stars kuwa imara uwanjani ili kulipigania Taifa lao kuhakikisha wanaondoka na ushindi.

 

“Kule kwetu Umasaini tuna vijana shupavu wanaitwa Morani, wale wanaua Simba na ni wakali kweli kweli, sasa hawa wachezaji wetu wageuke kuwa Morani pale uwanjani, kipigo walichokipata kule kwao (Cape Verde) iwe kama Simba amevamia zizi letu la ng’ombe, wamtoe na kumuua, hapana kuwa legelege.

 

“Nasikia TFF wameweka kiingilio cha shilingi 2000 kule kwa kawaida, mimi ningependa iwe 1000 ili watu waujaze uwanja ule kuwapa moyo Morani wetu,” amesema Lowassa.

JOTI: SIWALAUMU Wachezaji Stars/ Samatta na Ulimwengu Hawawezi

Comments are closed.