The House of Favourite Newspapers

Mmiliki wa Precision Air, Michael Shirima Afariki Dunia Jijini Dar es Salaam

0

 

Taarifa za kuhuzunisha zilizotufikia kwenye chumba chetu cha habari zimeeleza kuwa, mmiliki wa Kampuni ya Ndege ya Precision Air, Michael Ngaleku Shirima amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa, Mzee Shirima amefariki dunia usiku wa kuamkia hii leo Juni 10, 2023 alipokuwa akipatiwa matibabu hospitalini jijini Dar es salaam.

Imeelezwa kwamba Mzee Shirima alilazwa hospitalini tangu Juni 8, 2023.

Kifo cha Mzee Shirima kimethibitishwa na Kampuni ya Precision Air na kwa taarifa zaidi endelea kuwa karibu na GLOBAL TV.

Leave A Reply