Mnadhimu Mkuu Wa JWTZ Amkabidhi Zawadi Rais Wa Baraza La Michezo Ya Majeshi Duniani
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Haji Othman amemkabidhi zawadi Rais wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani (CISM) Kanali Nilton Gomes Rolim wakati wa hafla ya kuhitimisha Mkutano Mkuu wa Baraza hilo uliofanyika Jijini Dar Es Salaam.
Mnadhimu Mkuu amemwakilisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Jacob John Mkunda kuhitimisha hafla ya kufunga Mkutano huo wa 79 wa Baraza hilo tarehe 19 Mei 2024 ikiwa ni ishara ya ushirikiano kati ya JWTZ na Majeshi mengine Duniani.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu – JWTZ