Mnamibia wa Yanga awashtua Simba

ALICHOTAMKA Mnamibia wa Yanga, Sadney Urikhob lazima kiwashtue Simba. Amewaonya kwamba wasitarajie mteremko kutoka kwao kwani amejipanga kufanya maajabu msimu ujao kwenye mashindano yote.

 

Mshambuliaji huyo amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea PSM Medan ya Indonesia na tayari ameanza mambo kambini.

Sadney Urikhob

Akizungumza na Spoti Xtra, Urikhob alisema kuwa yupo nchini kwa kazi moja tu ya kuhakikisha anaipatia Yanga mafanikio huku akiwataka Simba wasahau suala la yeye kupita kwenye timu yao zaidi ya kuwasubiri uwanjani.

 

“Najua changamoto kubwa iliokuwa mbele yangu ni kuona timu yangu inafanya vizuri ikiwezekana kuchukua ubingwa hilo ndiyo jambo kubwa na muhimu kwa sababu umoja wetu ndiyo utatufikisha kwenye
malengo hayo, nitapamba na nimekuja kwa kazi hiyo.

 

“Sitaki kuwapa nafasi Simba, nafahamu ni wapinzani wa Yanga, nitawaheshimu kwa sababu ni timu kubwa, nimepita kwao japo hatukufikia muafaka, nadhani tutakutana uwanjani ndiyo sehemu itaonyesha ubora upo wapi,” alisema Urikhob

Loading...

Toa comment