MNAOSTAAJABU YA WEMA, ACHA NIWAKUMBUSHE YA GIGY!

NAJARIBU kuvuta picha siku ya kwanza kabisa kukutana na mwanadada anayefanya fresh kwenye game la muziki Bongo. Huyu si mwingine bali ni Gigy Money ambaye jina lake alilopewa na wazazi ni Gift Stanford.  Nakumbuka siku hiyo alikuja ofisini kwetu pale Bamaga -Mwenge jijini Dar kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano. Alikuwa amevaa suruali lainii ambayo ilikuwa ikimuonesha jinsi alivyoumbika. Hakika alikuwa na bonge shepu na ndiyo kitu ambacho kilimpa umaarufu mkubwa kipindi kile.

Kazi yake kubwa ilikuwa ni kupiga mapicha ya kihasara na kutupia kwenye mitandao, hata pale alipopata shavu la utangazaji kwenye vituo mbalimbali vya redio na televisheni, bado hakuishiwa na vituko vya kulipigia promo kalio lake. Lakini kuna wakati akapotea ghafla, alipokuja kuonekana, msambwanda wote ulikuwa umepuputika. Watu walishutushwa sana na ule muonekano wake na hapo ndipo yalipozuka maneno.

Kuna waliosema alikuwa akitumia dawa za Kichina ambazo zimeisha nguvu ndiyo maana amekongoroka, wengine wakasema eti alikuwa anaumwa, yaani ilimradi kila mmoja alisema lake. Licha ya watu kusema maneno mengi, Gigy hakuwa na la kuwajibu zaidi ya kuonesha kuukubali muonekano wake mpya. Akawa anapiga picha kama kawaida, wakati mwingine anajitahidi kujibinuabinua ili aonekana kuwa ana kijungu lakini watu walikuwa wakichukua picha zake za nyuma na za sasa kisha kuishia kuandika maneno ya kumsanifu.

Bahati nzuri sana Gigy hakujali maneno ya watu, aliendelea na maisha yake! Akaamua kubeba ujauzito na hatimaye akajifungua na sasa kijungu kinakuja kidogo lakini wengi wanaamini kuwa, Gigy wa miaka ile hawezi kurejea tena. Wakati zama za Gigy zikionekana zimeisha licha ya kwamba bado anajitutumua kimtindo, gumzo kubwa sasa hivi ni muonekano wa staa wa filamu Bongo, Wema Sepetu.

Sifa kubwa ya Wema tangu enzi zile aliposhiriki mashindano ya Miss Tanzania ni figa. Sina sababu ya kumuelezea sana Wema wa miaka ile kwani kila mmoja anajua alivyokuwa na msambwanda wa maana. Naye ghafla tukashangaa amekongoroka. Kupungua kwake kulimshitua kila mtu, hakuna aliyechukulia kama jambo la kawaida. Wengi walikuwa wakitaka kujua sababu ya kukonda kwake lakini ilikuwa ni ngumu kwani hakuweza kupatikana kueleza sababu.

Alichokuwa anakifanya ni kama vile alivyofanya Gigy, kupitia ukurasa wake wa Instagram akawa anatupia picha zikimuonesha akiwa kama mtoto huku mwenyewe akionekana kuufurahia muonekano wake mpya huyo.

Kama ilivyokuwa kwa Gigy, watu wakaanza kunong’ona kwamba eti ule msambwanda tuliokuwa tunauona kwa Wema enzi zile haukuwa OG, wakimaanisha hakuwa halisi bali wa Kichina. Ikaelezwa kwamba kuna dawa za Kichina ambazo ukitumia zinakuumua makalio yako lakini nguvu ya ile dawa ikiisha, mpododo nao unakwenda. Eti ndicho kilichompata Wema.

Wapo baadhi ya watu waliamini katika hilo lakini wengine wakasema eti naye anaumwa. Swali likawa; anaumwa nini? Hakuna aliyepata jibu la swali hilo. Wengine wakasema eti kilichomkondesha ni stress za kutendwa na wanaume pamoja na kutopata mtoto.

Kwa ufupi kwa hili la Wema yamesemwa mengi sana lakini ukweli ukawa umebaki moyoni mwake. Hata hivyo katika kuwatoa wasiwasi mashabiki zake, juzikati Wema aliongea na mmoja wa waandishi wetu na kuweka wazi sababu hasa zilizomfanya akonde.

Akasema: “Mimi nimekonda kwa sababu ya mawazo makali niliyokuwa nayo na si vitu vingine. Nilikuwa kwenye wakati mgumu sana ila siyo mbaya, kusema ukweli naufurahia huu mwili wangu wa sasa, nimekuwa sio mzito tena na navaa nguo ambazo nataka, tofauti na ilivyokuwa huko nyuma.”

Katika maelezo yake Wema alisema kuwa, kipindi alichopitia kwenye lile sakata la kuvuja kwa picha zake za chumbani na Patric Christopher ‘PCK’ kilikuwa kigumu mno kwani alikuwa anapitisha hata siku tatu bila kula chochote mpaka anapepesuka.

Kwa maana nyingine tukubali tu kwamba, kilichomfanya staa wetu huyu akonde ni matatizo aliyokumbana nayo katika siku za hivi karibuni na kwa sababu anajua kabisa ule mshepu wake hauwezi kurudi tena ndiyo maana imebidi ajikubali vile alivyo.

Ila ukweli unabaki palepale kwamba, Wema wa sasa akipita mbele za watu hashitui sana kama Wema yule wa miaka ile. Kama ilivyo kwa Gigy Money ambaye ule msambwanda wake umeyeyuka na sasa amebaki kujibinuabinua ili angalau kuonekana kwamba bado umo lakini ukweli ni kwamba hamna kitu.


Loading...

Toa comment