Mnataka kulia? Gadiel tayari mali ya Simba

KLABU ya Simba, imemtambulisha beki wa kushoto, Gadiel Michael baada ya kukamilisha usajili wake kwa kumpa mkataba wa miaka miwili. Gadiel ametua Simba akitokea Yanga baada ya kuitumikia timu hiyo kwa misimu miwili ambapo alikuwa mchezaji tegemeo katika nafasi ya beki wa kushoto.

 

Kukamilika kwa usajili huo, ni dhairi sasa mchezaji huyo wa zamani wa Azam FC, anaenda kupambania nafasi na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye ni Nahodha Msaidizi wa Simba.

Picha ambazo jana mchana zilisambaa katika mitandao mbali-mbali, zilimuonyesha mchezaji huyo akiwa na Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori wakati anasaini. Usajili huo wa Gadiel umekuja ikiwa ni siku chache baada ya Simba kuzinasa saini za Ibrahim Ajibu na Beno Kakolanya ambao wote walikuwa wakiitumikia Yanga msimu uliopita.

Wengine wapya ambao tayari wamejiunga na Simba kipindi hiki ni Kennedy Juma kutoka Singida United, Francis Kahata (Kenya), Deo Kanda (DR Congo), Sharaf Eldin Shiboub Ali Abdalrahman (Sudan), Tairone Santos da Silva, Gerson Fraga Vieira na Wilker Henrique da Silva ambao wote ni raia wa
Brazil

 

Wengine ni Ibrahim Ajib ambaye alikuwa nahodha wa kikosi cha Yanga pamoja na Beno Kakolanya ambaye alikuwa ni mlinda mlango wote wamesaini kandarasi ya miaka miwili.

 

Loading...

Toa comment