MNC wa PSG Waitikisa Dunia

Neymar, Kylian Mbappe na Edinson Cavani washambuliaji hatari zaidi duniani kwa sasa.

 

TAYARI PSG imeshaonekana kuwa na safu ya ushambuliaji hatari zaidi duniani kwa sasa, ukiachana na zile za timu kadhaa zilizopo kwa sasa. Huwezi kutaja safi bora za ushambuliaji Ulaya ukaacha kuitaja safu hiyo ya PSG ambayo ina washambuliaji hatari watatu, Neymar aliyejiunga na timu hiyo akitokea Barcelona, Kylian Mbappe aliyejiunga nao akitokea Monaco na Edinson Cavani ambaye alikuwa kwenye timu hiyo tangu msimu uliopita.

 

Wanaume hawa watatu ambao wanaunga umoja wao NMC, wameshaanza kuonyesha kuwa wao ni watu hatari na wanaweza kufanya jambo lolote kubwa kwenye michuano yote msimu huu. Tayari wameshakuwa hatari Mnc waitikisa duniakwenye Ligi Kuu ya Ufaransa, Ligue 1 na karibia mabao yote waliyofunga wao wamekuwa wakishiriki pamoja.

Kylian Mbappe aliyejiunga nao akitokea Monaco

Wikiendi iliyopita walifanikiwa kuongoza mauaji ya mabao 5-1 dhidi ya Metz, huku Cavani akifunga mabao mawili na Neymar moja. Huu ulikuwa mchezo wa kwanza kwa Mbappe kuichezea timu hiyo ambayo imefanikiwa kushinda michezo yake yote minne msimu huu.

 

Mbappe alifanikiwa kuifungia timu hiyo kwenye mchezo wake wa kwanza tangu alipojiunga nayo akionyesha kuwa anaweza kwenda na kasi ya timu hiyo. Mbali na kuwa hatari kwa kufunga mabao, lakini hii ndiyo inatajwa kuwa safu ya ushambuliaji ghali zaidi kwa sasa kwenye soka duniani. Mbappe, alijiunga na timu hiyo kwa kitita cha pauni milioni 166, ikitajwa kuwa msimu huu anacheza kwa mkopo lakini mwakani atatakiwa kusajiliwa jumla. Neymar mtoto wa Kibrazili alijiunga nao kwa kitita cha pauni milioni 198, kwa sasa ameshacheza michezo minne na yote ameonyesha kiwango cha hali ya juu sana kwenye timu hii.

 

Lakini ukweli ni kwamba thamani ya Cavani kwa sasa ni kitita cha pauni milioni 55, baada ya kusaini mkataba wa miaka minne kwenye timu hiyo jambo ambalo linaonyesha kuwa hii ndiyo safu ghali zaidi ya ushambuliaji duniani kwa sasa. Hata hivyo, pamoja na kwamba walionekana kucheza kwa ushirikiano mkubwa wachezaji hao wote watatu, lakini timu hiyo imepewa onyo kuwa inatakiwa kuhakikisha inaweka sawa safu yake ya ulinzi ambayo haionekani kuwa imara. PSG wanaweza kufunga mabao matano na kufungwa matano kutokana na aina ya mabeki ambao wanao kwa sasa.

 

Lakini wanatakiwa kusubiri kuona nini kitatokea pale watakapoingia kwenye michuano mikubwa duniani ikiwemo ile ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo watakutana na vigogo kama Juventus, Barcelona, Real Madrid, Chelsea na Manchester United kuona kama wanaweza kuepuka gundu ambalo limekuwa likiwaandama kwa miaka mingi la kushindwa kufanya vizuri kwenye michuano hiyo.

Kitendo cha Monaco ambao ni mabingwa watetezi kufungwa na Nice kinaonyesha kuwa PSG watarejea tena kwenye nafasi yao ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa miaka kadhaa tena wakiwa na safu hiyo hatari. Hadi sasa Ulaya nzima Cavani anashika nafasi ya pili kwa kufunga mabao kwenye ligi zote akiwa ameshaweka kambani mabao matano. Kwa pamoja watatu hao wameshafunga mabao kumi wakionekana kuwa ndiyo hatari zaidi, huku Neymar akifunga manne na Mbappe moja.

MONACO, Ufaransa


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment