POLISI nchini Kenya wamemkamata raia wa Nigeria, Henry Omoaka (51) akiwa na Dola feki za Marekani 251,4000 ambazo ni sawa na Sh. milioni 25.3 za Kenya.
Omoaka ambaye alisema ni mwandishi wa filamu na aliyekuwa na hati za uhamiaji zilizokwisha muda wake, na aliyekamatwa katika eneo la South B jijini Nairobi alisema alifanyiwa njama hizo na watu fulani wa Kenya na Nigeria.
Mtu huyo ambaye anaishi katika nyumba peke yake, alikana kuhusika na fedha hizo.
Tukio hilo limetokea siku mbili baada ya polisi kuwakamata raia wawili wa Chad na dereva wao Mkenya eneo la Westland, Nairobi, wakiwa na fedha feki za thamani ya Sh. bilioni moja zikiwa ni Dola za Marekani na Euro.
Fedha hizo zinaaminika kutumika kutapeli Wakenya.
Credit: The star
Comments are closed.