Mnyama Anguruma Nigeria, Ampiga Plateua Utd 1-0
Mabingwa wa Tanzania timu ya Simba leo Novemba 29, imefanikiwa kushinda mchezo wake wa kwanza kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ugenini, kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Plateua United, mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja New Jos, Nigeria wenye uwezo kuchukua watazamaji 40,000.
12
Goli pekee la wekundu wa msimbazi liliwekwa kimiani na mchezaji wa kimataifa wa Zambia, Cloutus Chama dakika ya 53 kipindi cha pili, akipokea pasi ya Luis Miquissone ambaye alikuwa ni hatari kwa mabeki wa Plateau United.
Mchezo huo uliochezwa uligubikwa na matukio mengi kutoka kwa wenyeji wakiwa na lengo na kuwatoa Simba mchezoni, mojawapo ya tukio kubwa ilikuwa kugoma kutoa kibali mechi hiyo kuonyeshwa kwenye runinga kupitia kituo chochote cha habari.
Baada ya ushindi huo ambao kikosi cha Simba kinarejea nchini kujiandaa na mechi ya marudiano itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es salaam, Desemba 6.