The House of Favourite Newspapers

Mnyika Awatahadharisha CHADEMA Mauaji ya Kutisha- Video

KAIMU Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, amewatahadharisha viongozi wa chama hicho na wananchi kuhusu mauaji ya kutisha ambayo yanatokea hapa nchini.

Mkutano na wanahabari ukiendelea.

 

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Feb 23, 2018, Mnyika amesema viongozi wa Chadema wanapaswa kuchukua tahadhari  kwani vifo vingi na vya kutatanisha vimetokea siku za hivi karibuni huku wengi wa waliouawa wakiwa ni viongozi wa chama hicho.

 

“Kumekuwa na mfululizo wa matukio ya viongozi wa Chadema kuuawa, waliomteka, kumtesa na kumuua  katibu wa chama hicho kata ya Hananasifu jijini Dar es Salaam, Daniel John;  Godfrey Luena ambaye ambaye tumelezwa baada ya kukatika umeme  alipotoka,  akashambuliwa na kuuawa usiku wa kuamkia leo. Katika mazingira kama haya, tunatoa wito kwa viongozi wa Chadema nchi nzima,  kwa wabunge na madiwani kuchukua tahadhari kubwa na kujilinda,” amesema Mnyika.

 

“Mambo haya yamefikia kwa wanahabari, Azory Gwanda wa Mwananchi  na  mpaka sasa hajulikani alipo,  na Emmanuel Kibiki wa Raia Mwema wa Makambako Njombe ambaye naye alikamatwa. Hizi ni ishara kwamba katika taifa letu kuna vikundi vya watekaji, watesaji na wauaji,” alisema Mnyika.

TAZAMA VIDEO YA TUKIO HILO

Comments are closed.