The House of Favourite Newspapers

Mo aanza na uwanja Simba SC

BAADA ya afya yake kuimarika, mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ ameanza na ishu ya maendeleo ya uwanja wa timu hiyo unaojengwa Bunju jijini Dar es Salaam na akatoa maagizo.

 

Licha ya kwamba maagizo hayo yanashtusha lakini yanasikitisha. Mo ambaye ni mwanachama wa Simba, ameanza ujenzi wa uwanja huo mara baada ya kukamilika kwa mchakato wa klabu hiyo kuingia katika mfumo wa kampuni mapema mwaka huu.

Mo alieleza maendeleo ya uwanja huo kupitia kurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram wenye mashabiki 697,000 ambao alitoa maneno hayo ambayo yaliyosomeka hivi: “Tumefika hatua nzuri ya maendeleo ya uwanja wetu wa Simba nafurahi kuona maono yangu yanakamilika ili hata siku nisipokuwepo duniani, uwanja uendelee kutumika kwa mazoezi InshaAllah.”

 

Kiongozi huyo ambaye takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kwamba ameajiri zaidi ya watu 23,000 nchini, alianza ujenzi huo wa uwanja mwezi uliopita lakini hapo katikati alipata matatizo baada ya kutekwa Oktoba 11, mwaka huu akiwa anaingia gym asubuhi kufanya mazoezi na alipatikana Jumamosi iliyopita katika eneo la Viwanja vya Gymkhana jijini Dar.

Licha ya kiongozi huyo kutoweka hapa katikati lakini ujenzi wa uwanja huo ulikuwa ukiendelea na ikiwa ni moja kati ya ahadi ambazo aliahidi ataweza kuwatimizia Simba.

 

Msimu huu mpya Mo ndiye aliyefanikisha usajili wa klabu hiyo kuwa kuwanasa wachezaji mahiri pamoja na kuweka benchi la ufundi jipya na ndiye amekuwa akishughulikia mambo ambayo yanaendelea ndani ya Simba kwa sasa ingawa uchaguzi unafanyika mwezi ujao rasmi.

MARTHA MBOMA, DAR ES SALAAM

Comments are closed.