Mo Amchenjia Chama Kisa Manara Insta!

STAA wa Simba, Clatous Chama Agosti 6, 2021 ameonja joto la jiwe baada ya kuchenjiwa kibao na muwekezaji wa klabu hiyo, Mo Dewji kisa Haji Manara.

 

Chama akiwa Live Insta kwenye mkutano wake na mashabiki ambao Mo alikuwemo, aliulizwa swali kuhusu kuondoka kwa Haji Manara ndani ya klabu ya Simba, kwenye kujibu Chama alimsifia Haji kitendo ambacho kilionekana kumchefua sana Mo.

Mo alimuuliza Chama “Haji ndiye aliyekulipia ada ya uhamisho?” Chama akiwa anamjibu Mo alijibu kwa kuomba msamaha kama amemkwaza, Mo akamuuliza tena Nani aliyekulipa Ada….Haji? baadae Chama alipotaka kujibu Mo akamwambia anatoka kwenye mkutano huo.704
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment