The House of Favourite Newspapers

Mo Ashusha Straika Matata Simba SC

0

WAKATI wadau wa michezo wakiendelea kutega sikio kwenye hukumu ya aliyekuwa nyota wa Yanga, raia wa Ghana, Bernard Morrison, huku Simba mambo yanazidi kunoga.

 

Kesho Alhamisi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Mohamed Dewji ‘MO’, anatarajiwa kushuka na mbadala wa Meddie Kagere, Justin Shonga raia wa Zambia.

 

Mo anatarajiwa kutua mapema kesho akitokea Dubai, ambapo alienda kwa ajili ya shughuli zake na kukwama kurejea nchini kufuatia tatizo la mipaka mingi kufungwa kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona, lakini pamoja na hayo Mo, anatarajia kutua na straika anayekipiga katika Klabu ya Orlando Pirates ya nchini Afrika Kusini, Justine Shonga.

Straika huyo mkataba wake na Orlando Pirates, unadaiwa kumalizika tangu Juni 30 mwaka huu, huku akisuasua kuongeza kwa miamba hao jambo ambalo liliwafanya Simba na Yanga kuongeza nguvu ya kuwania saini yake, huku Simba akidaiwa kufanikiwa kumshawishi kutua nchini.

 

Chanzo chetu cha ndani ya Simba kililiambia Championi Jumatanokuwa, ni kweli timu hiyo imefanya usajili wa wachezaji kadhaa katika dirisha hili lakini usajili wa Shonga unamhitaji mwenyekiti kwa kuwa ni usajili wa fedha nyingi tofauti na wachezaji wengine ambao wameshaanikwa hadi sasa.

 

“Kimsingi sisi hadi sasa usajili wa wachezaji ambao tumeufanya ulisimamiwa na baadhi ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi, lakini huu wa Shonga tunamsubiri mwenyekiti mwenyewe aje kwa kuwa unahitaji fedha nyingi mpaka ukamilike.

 

“Shonga tumeshafi kia kwenye mazungumzo ya mwisho na ndiyo maana nakuambia atatua kesho au keshokutwa na mara tu Mo atakapotua, kwani kwa sasa hana mkataba ndani ya Orlando Pirates,” kilisema chanzo.Shonga mwenye umri wa miaka 23, msimu huu ndani ya Orlando amefanikiwa kufunga mabao matano na kutoa pasi mbili za mabao katika michezo nane aliyocheza.

Leave A Reply