The House of Favourite Newspapers

Mo Dewji amshusha wa kumzuia Balinya

MABOSI wa Simba wameamua kuwalipa wenzao wa Yanga ambao walikuwa wanatamba na straika mpya, mganda, Juma balinya baada ya kumshusha mtu wa kumzuia. Mashabiki wa Yanga tangu Jumamosi iliyopita walikuwa wanatamba baada ya kumsajili straika wao mpya, Juma Balinya ambaye ametokea Polisi ya Uganda.

 

Straika huyo ametua Yanga baada ya kufunga mabao 19 msimu uliopita. Mabosi hao wa Simba ambao wanahusika na Kamati ya Usajili wakiongozwa na mwekezaji wao Mohammed Dewji ‘Mo’ jana Jumanne walimtangaza rasmi beki mwili jumba, Kennedy Juma kutoka Singida United kuwa beki ambaye atakuja kumzima straika huyo wa Yanga. Kennedy anakuwa mchezaji wa pili mpya kusajiliwa na klabu hiyo baada ya Beno Kakolanya ambaye alikuwa huru baada ya kuvunjwa kwa mkataba wake na Yanga.

 

Kennedy ambaye alikuwa nahodha wa Singida United, amesaini mkataba wa miaka miwili wa kujiunga na kikosi hicho cha Simba kinachofundishwa na kocha Patrick Aussems raia wa Ubelgiji.

 

Kennedy anaungana na wachezaji Kakolanya, Aishi Manula, John Bocco, Meddie Kagere, Jonas Mkude na Erasto Nyoni kuwa nyota ambao wamesaini mikataba katika klabu hiyo hadi sasa. Kennedy anaongeza idadi ya mabeki ndani ya kikosi hicho ambacho hadi sasa kina Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Yusuph Mlipili na Paul Bukaba.

 

Said ally, Dar es Salaam

 

Comments are closed.