Mo Dewji Awatuliza Munkari Wapenzi wa Simba

BAADA ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu hiyo, Mohammed Dewji (Mo) kutangaza kuachia ngazi kutokana na kutoridhishwa na matokeo ya Simba kupoteza taji la kwanza msimu huu baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar, katika fainali ya Kombe la Mapinduzi uwanja wa Amani.

Leo kupitia ukurasa wake wa instagram na twitter amesema haya:- “Kilichotokea kwenye akaunti zangu jana kilikuwa ni bahati mbaya, tuko pamoja, tunarudi kwenye ligi tukiwa na nguvu , tunajipanga kwa ajili ya ligi, nawapongeza Mtibwa kwa kuchukua kombe, mimi ni Simba damudamu, nitabaki kuwa Simba”.

Alichokuwa amekisema siku ya jana:- Mo alisema: “Baada ya kulipa mishahara inayofikia Sh4 bilioni kwa mwaka, najiuzulu wadhifa wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi. Nitabaki kuwa mwekezaji na nitazingatia kukuza miundombinu ya soka la vijana.”

 

 


Loading...

Toa comment