Mo Dewji: Niliamua Kurudi Katika Uongozi Kuleta Msukumo Mpya
Rais wa Simba, Mohammed Dewji Oktoba 6, 2024 amesema katika Mkutano Mkuu wa Klabu ya Simba mwaka 2024 uliofanyika jijini Dar es Salaam kuwa leo ni siku ya heshima kubwa kuangalia maendeleo ya timu yao katika safari yao ya maendeleo ndani ya klabu hiyo.
“Nilipoamua kurudi katika uongozi kwa ajili ya kuleta msukumo mpya katika maono yetu ya safari yetu ya mafanikio ya baadae.”
“Kujenga Simba mpya inagharama kubwa lakini tunaenda kupambana kujenga kikosi imara ambacho kitaweza kuleta ushindani, ikiwemo usajili wa Elie Mpanzu.”
“Tutahakikisha kila hatua tutachukuwa kwa umakini mkubwa sana, kwa pamoja tunajenga Simba kuwa endelevu na kufika katika safari yetu kila mmoja wenu kushirikiana katika kujenga Simba mpya.”
Mradi mkubwa ambao utaweka msingi wa mafanikio yetu baadae. Tunatarajia kujenga kambi bora ya mazoezi itakuwa na gym, majengo ya malazi, kituo cha lishe, bwala la kuogolea, kituo cha burudani, viwanja vitano vya kisasa zaidi ya hayo kujenga makumbusho ya klabu na kuanzisha chuo cha maendeleo ya vijana ili kulea vipaji vya soka nchini.”- moodewji.