The House of Favourite Newspapers

MO Jeuriii! Simba Kupiga Kambi Nzito Uturuki

MICHUANO ya Kagame ikimalizika tu, Simba wanakwea pipa kwenda Uturuki kambini kutuliza akili kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu na michuano yakimataifa.

 

Ligi Kuu inaanza Agosti huku Ligi ya Mabingwa Afrika ikianza Novemba mwaka huu. Hiyo itakuwa ni mara ya pili mfululizo kwa Simba kuweka kambi nje ya nchi baada ya kwenda Sauzi msimu uliopita wakati kikosi hicho kilipokuwa chini ya kocha Joseph Omog raia wa Cameroon.

 

Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba ambayo inapewa nafasi kubwa ya kubeba Kagame, zinasema mikakati ya kuweka kambi hiyo imekamilika na ni moja ya mipango ya Mohammed Dewji ‘MO’ kuhakikisha kwamba Simba inakuja na mabadiliko makubwa msimu ujao.

 

“Tayari wachezaji wameshapewa taarifa kuhusiana na kambi hiyo na jana (juzi) waliambiwa wakusanye pasipoti zao kwa ajili ya kuanza kwa taratibu ya kwenda nchini humo.”

 

Alipoulizwa kuhusiana na hilo Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Masoud Djuma alisema kuwa hana taarifa juu ya ila anajua kuwa kulikuwepo na mpango wa timu hiyo kwenda kupiga kambi nje ya nchi lakini hajui ni nchi gani.

Comments are closed.