The House of Favourite Newspapers

Mo Music achekelea kuwa huru kesi ya utapeli

0

Na Gladness Mallya

MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva, Moshi Katemi ‘Mo Music’ hivi karibuni alijikuta akitoa meno yote nje kutokana na furaha aliyokuwa nayo baada ya kuambiwa na mahakama yupo huru katika kesi ya utapeli iliyokuwa ikimkabili.

Akizungumza na mwandishi wetu juzi, Mo Music alisema: “Namshukuru Mungu sana kwa sababu sasa nina amani tele maana hii kesi ilikuwa inaniumiza sana kichwa na kushindwa kufanya mambo mengine ya maendeleo, niko huru baada ya kesi kusomwa katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma na hakimu kusema sina hatia.”

Mo Music alikuwa mshtakiwa namba mbili wa kesi ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu baada ya kuhusishwa na mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Joyce Ngerangere aliyekuwa mpenzi wake ambapo alidaiwa alimtapeli mamilioni mwanaume aliyejulikana kwa jina la Barthazar aliyekuwa mpenzi wake.

Leave A Reply