The House of Favourite Newspapers

MOBETO ACHARUKA, KISA DIAMOND

Hamisa Mobeto

MWANAMITINDO Hamisa Mobeto juzikati alicharuka kinoma baada ya kuulizwa kuhusiana na madai ya mzazi mwenzake Nasibu Abdul ‘Diamond’ kusitisha huduma za matunzo ya mwanaye Dylan.  Awali, chanzo makini kililitonya Risasi Jumamosi kuwa, Mobeto kwa sasa anahaha baada ya kukosa matunzo kutoka kwa mzazi mwenzake huyo ambaye amesitisha mgao wa matunzo.

“Mnajua Mobeto na Diamond kwa sasa ndiyo haziivi kabisa kwani amefikia hatua ya kushindwa kupewa matumizi ya mtoto, bi dada anahaha hajui la kufanya,” kilisema chanzo. Aidha, chanzo hicho kilidai kuwa, Mobeto kuna wakati anatamani hata angekuwa anapatana na mama wa Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ angeweza kumsaidia.

“Si unajua tena familia nzima ya akina Diamond hapatani nayo hivyo hawezi kupata msaada kwani kuna wakati huwa anajisemea kuwa anatamani angekuwa hata anaongea na Bi Sanura angemsaidia,” kilisema chanzo hicho. Baada ya chanzo hicho kumwaga ubuyu huo, mwandishi wetu alimwendea hewani Mobeto ambaye alicharuka vibaya na kumpa makavu akidai kuwa hataki kabisa kusikia habari zinazomhusu Diamond.

“Nyie nanyi mnachosha, sasa kama ameacha kutoa huduma kwa Dylan inawahusu nini? Niacheni bwana, maisha yangu na familia haiwahusu mnauliza ili iweje?” alihoji Mobeto na kukata simu. Huko nyuma, Mobeto aliwahi kumburuza Diamond mahakamani kutokana na suala hilo la ‘kukacha’ kutoa matunzo lakini hata hivyo walipofika mahakamani walilimaliza kabla ya hivi karibuni kuibuka upya.

STORI: Memorise Richard, Risasi Jumamosi

Comments are closed.