MOBETO AFICHUA SIRI YA MAFANIKIO YAKE

MWANAMITINDO maarufu na pia mwanamuziki Bongo, Hamisa Mobeto amesema siri kubwa iliyomfanya aweze kupiga hatua maishani ni kuziba masikio na kujifanya kama hasikii yanayosemwa kumhusu yeye.

 

Akizungumza na Amani, Mobeto alisema kuwa changamoto alizokutana nazo na maneno mengi ya watu kwenye mitandao ya kijamii, kama angezisikiliza basi ni wazi asingeendelea kimaisha.

 

“Siku zote kama utaamua kutazama watu wanasema nini kuhusu wewe lazima utafeli, niliweka kando kelele zao sijui kuhusu ushirikina, sijui mambo ya Diamond na sasa namshukuru Mungu anazidi kunibariki,” alisema Hamisa ambaye sasa hivi amepata madili mbalimbali

Stori: Imelda Mtema


Loading...

Toa comment