MOBETO AKOLEZA SKENDO YA KUFUMANIWA ZANZIBAR

Hamisa Mobeto

SIKU chache baada ya mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Mobeto kukutwa na skendo ya kufumaniwa na bwana wa mtu ambaye jina lake linahifadhiwa kwa sasa, mwenyewe ameibuka na kukoleza fumanizi lake hilo, Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili.  

 

Mobeto alidaiwa kufumaniwa na bwana wa mrembo anayejulikana kwa jina la Tahiya ambaye aliposti picha ya Mobeto kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika maneno haya; “Hamisa Mobeto achana na wanaume za watu.”

 

Baada ya muda mwanadada huyo akaposti tena meseji zao zote alizokuwa wakijibizana na mwanamitindo huyo kwenye mtandao wa WhatsApp ambapo Tahiya alionekana akimsihi Mobeto aachane na mpenzi wake lakini haikusaidia kwani mwisho wa waliishia kujibizana maneno mabaya huku kila mmoja akijiona anaweza zaidi ya mwenzake.

 

MOBETO AKOLEZA SKENDO

Baada ya skendo hiyo kutikisa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, Risasi liliamua kumtafuta Mobeto ambaye alilikoleza fumanizi hilo kwa kutoa maneno ya shombo.

“(Kwa sauti ya ukali) Mnataka niwaambie nini, mlichokiona ndiyo hichohicho isitoshe mimi siyo mtoto mdogo kwa hiyo naelewa ninachokifanya, sijaiba mwanaume wa mtu ila alikuja mwenyewe na nampenda nifanyeje sasa,” aliongea Mobeto na kukata simu.

 

Kwa upande wa mama mzazi wa Mobeto, Shufaa Lutiginga alipotafutwa ili azungumzie kuhusu skendo hiyo ya mwanaye kufumaniwa na bwana wa mtu alilipuka na kusema mwanaye aachwe aishi anavyopenda mwenyewe.

“Jamani nilishawaambia muacheni Hamisa aishi vile ambavyo yeye anapenda, msimfuatilie siku akihitaji kuongea na nyie atawatafuta yeye mwenyewe lakini siyo kila kukicha kumfuatilia,” alisema mama Mobeto.

Stori: MEMORISE RICHARD, RISASI MCHANGANYIKO

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Toa comment