The House of Favourite Newspapers

Mobeto: Lulu kanipora bwana!

0

fcvMwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Hassan Mobeto.

MAPENZI ya mjini utata mtupu! Ni kauli inayostahili kutumika baada ya mwanamitindo maarufu Bongo, Hamisa Hassan Mobeto kumwaga chozi akidai kuporwa bwana’ke aliyekuwa akimpa jeuri mjini (jina tunalo) huku zigo la lawama likimwangukia staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

CHANZO KINASEMAJE?
Habari kutoka kwa chanzo makini zilieleza kwamba, kwa sasa kuna bifu jipya linalotokota mjini likihusisha sakata la Lulu kumpiku Mobeto kwa bwana’ke aliyekuwa akimgharamia kiasi cha kuwa mwanaume pekee aliyemwamini hadi kufikia hatua ya kumzalia mtoto.

iklmmStaa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Ilidaiwa kwamba, jambo hilo Lulu hakulithamini na kuamua kumpiku huku akimuacha akiishia kulalama kila kukicha.

“Najua hamuujui mchongo huu. Sasa ngoja niwapashe habari kwa kina. Nimeamini Lulu kweli ni jasiri, maana kwa alichomfanyia Mobeto Mungu ndiye anajua.

PEDESHEE MPYA WA LULU?
“Huwezi kuamini yule bwana wa Mobeto Lulu kaamua kujiweka kwake, inaweza kuwa ngumu watu kukubali lakini ndiyo ukweli wenyewe.

“Unaambiwa mtiti wa Mobeto na Lulu ulianza kama mwezi mmoja uliopita. Walianza kwa kuandikana kwa mafumbo kama waimba taarab kwenye mitandao ya kijamii.

MAFUMBO INSTAGRAM
“Nimekutana na rafiki wa Mobeto ndiye kanipa mkanda wote kuwa Lulu kampiku Mobeto kwa bwana’ke ndiyo maana mafumbo hayaishi Instagram.

MOBETO HATAKI KUMSIKIA LULU
“Kwa sasa Mobeto hataki kusikia habari za Lulu na ukimuuliza anasema Mungu atamlipia kwani anamshukuru kumtoa huko kwani alipo sasa ana amani tele,” kilidai chanzo hicho.

MOBETO AFUNGUKA MAZITO
Kwa upande wake, Mobeto alipoulizwa juu ya sakata hilo alisema kuwa kwa sasa ana mambo yake mengine hivyo habari za Lulu ingekuwa vizuri akaulizwa yeye na huyo bwana’ke.

Mobeto alisema kuwa kwa sasa anachoweza kuzungumzia ni juu ya maisha ya mama yake mzazi na mtoto wake kwani hao ndiyo faraja pekee iliyobaki kwake.

Alisema kuwa, hapendi kuzungumzia mambo yaliyopita kwani kila jaribu lina mlango wake wa kutokea hivyo yawezekana yote Mungu aliyapanga akiwa na sababu za msingi.
“Mambo hayo mimi sitaki hata kuyazungumzia kwa sasa, nafikiri ingekuwa vyema ukamuuliza Lulu na ….(anamtaja huyo mwanaume) kwani wao ndiyo wanaweza kukupa ukweli na kukusimulia kiunagaubaga.

MOBETO AMWACHIA MUNGU
“Katika maisha yangu, kwa sasa namwangalia mtoto na mama yangu, hao wakikosa furaha hata mimi siwezi kuwa na amani kwenye maisha yangu, kwani mambo mengine yakishapita hakuna sababu ya kuyaendeleza zaidi namshukuru Mungu.
“Kwa sasa nina michongo yangu mipya na siko tayari tena kuzungumzia habari nje ya familia yangu.

“Ninachoweza kukuambia ni kwamba maisha yana kila staili ya kuishi hivyo sifikirii tena kuingia kwenye mitandao ya kijamii kuzungumzia habari za mtu kwani hata hao wanaonizungumzia sina muda wa kuanza kusoma comments (maoni) zao wala kuwajibu.

“Kwa kifupi sijawahi hata kuona mambo yanayozungumzwa kuhusu mimi kwenye mitandao maana huwa sisomi tena kwani kila mtu ana namna ya maisha aliyochagua.
“Hata huyo Lulu na timu zake mimi sina muda wa kusoma mambo yao kwani Mungu ndiye tegemeo langu,” alisema Mobeto.

LULU ARUKA MITA MIA
Alipotafutwa Lulu na kupewa taarifa za uporaji wa bwana wa mtu, aliruka mita mia moja kwa kusema kuwa habari hiyo ni mpya kwake na hajawahi kusikia lolote ila ndiyo anaambiwa kwa sasa hivyo kama kuna mtu ana picha zake na huyo bwana wa Mobeto, basi ndiyo anapata taarifa.

“Madai haya kwangu ni mapya na siyajui ndiyo mnaniambia kwa mara ya kwanza, sioni sababu ya kulizungumzia,” alisema Lulu.

Leave A Reply