Mobeto Na Zari Nyota Zao Zinaendana

Hamisa Mobetto

WIKI hii ilikuwa ‘busy’ sana na masuala mbalimbali yaliyotokea kwenye kinyan- g’anyiro cha Shindano la Miss Tanzania 2018, ambapo mrembo kutoka Kinondoni Queen Elizabeth aliibuka mshindi.

 

Tupate ‘break’ kidogo kutoka Miss Tanzania na tucheki ishu nyingine zinazoendelea duniani ingawa kwa namna moja au nyingine zinaweza kugusa kwa kiasi kidogo kwenye mambo ya ma-miss.

 

Sasa kabla ya shindano la ma-miss kufanyika Jumamosi, kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram kulichafuka na hiyo ilikuwa ni baada ya mrembo kutoka Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kuweka ujumbe kwenye mtandao wa kijamii akionyesha mahaba yake kwa Mobeto zaidi akimtia moyo kuzidi kupambana ili kufika mbali zaidi.

 

Kwenye ujumbe wake Zari hakuandika jina Mobeto, watu walijio-ngeza tu lakini pia gazeti dada la hili la Risasi liliz-ung-umza na Zari akathi-bitisha kwa-mba ni kweli uju-mbe ule ulik-uwa ni kwa Mo-beto.

 

Ina-weza kuwasha-ngaza wengi kuona Zari anatoka hadharani na kuonyesha mahaba kwa Mobeto, lakini kwa taarifa yako nyota za wawili hawa ni kama zinaendana hivi, kwa sababu mambo mengi wanakwenda pasu kwa pasu (nusu kwa nusu). Nitakuchambulia zaidi;

 

Kualikwa kwenye mashindano ya ma-miss

Kwenye kinyang’anyiro cha Miss Tanzania 2018, kilichofanyika Jumamosi iliyopita pale kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere, Mobeto alikuwa ni mshereheshaji ‘MC’ akisaidiana na mtangazaji wa East Africa Televisheni, Deogratius Kithama.

 

Kama hufahamu, kwa upande wa Zari kwenye kinyang’anyiro cha Miss Uganda 2018, kilichofanyika mwezi uliopita kwenye Hoteli ya Sheraton jijini Kampala ambapo mrembo Quiin Abenakyo alishinda, alialikwa kuwa jaji kwenye mashindano hayo.

Kuzaa na mwanaume mmoja

Zari na Mobeto wanakutana mahali hapa tena. Wote wana watoto kutoka kwa mwanaume mmoja ambaye ni staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Tofauti na watu wengi ambavyo wangetegemea kuona wawili hawa wanakuwa maadui kutokana na kuchangia penzi, Zari ‘kawa-prove’ wengi ‘wrong!’.

 

Kuzaa na wana-ume tofauti maa-rufu

Mbali na kuzaa na mwanaume mmoja ambaye ni Diamond, wote wawili wana watoto kutoka kwa wanaume wengine maarufu. Zari alizaa watoto watatu na marehemu mume wake, Ivan Semwanga ambaye alikuwa ni maarufu Uganda na South Africa, lakini Mobeto pia amezaa na bosi wa redio, anayefahamika zaidi kwa jina la Majizo.

 

Biashara

Zari yupo mbele kwa Mobeto kwenye masuala ya biashara na bila shaka anaingiza mkwanja mrefu kuliko mwanamitindo huyu. Ana miliki biashara mbalimbali zikiwemo shule pamoja na hosteli za kuishi wanafunzi, kwa upande wa Mobeto yeye anamiliki duka la nguo. Lakini wote kwa pamoja ni wafanyabiashara.

 

Hivyo ni baadhi ya vitu au matukio ambayo yamewafanya wawili hawa kutoka pasu kwa pasu, pengine mbeleni kuna mengi yataongezeka, nani ajuaye? Yajayo yanafurahisha sana!

BONIPHACE NGUMIJE

Loading...

Toa comment