MOBETO: NJOONI DAR LIVE KESHO MPATE BURUDANI – VIDEO

Mmoja wa waandaaji wa tamasha hilo, Victor Kaduma (katikati) kutoka LBM Entertainment akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo katika ofiza za Global Group zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Mr. Blue na Mobeto.

MWANAMITINDO na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto, amewaambia mashabiki wake kujitokeza kwa wingi kesho Jumatatu kwenye Ukumbi wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhiem kupata burudani kutoka kwake.

 

Mobeto ameyasema hayo leo Jumapili  Agosti 11, 2019 mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za Global Group zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam ikiwa imebaki siku moja kuelekea kesho Jumatatu katika Sikukuu ya Idd, ambapo kutakuwa na tamasha baab’kubwa lililopewa jina la Bonsi Vibe likiwakutanisha Bongo Fleva na Singeli.

Mobeto akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), pembeni yake ni mratibu na meneja wa Dar Live, Rajabu Mteta ‘KP Mjomba’.

“Kikubwa watu watarajie burudani kali kutoka kwangu, watu waje kwa wingi niwape burudani bila kikomo.

“Najua wengi wana hamu ya kumuona Mobeto, hivyo fursa ndiyo hii na siyo ya kukosa kabisa kwani kwa mara ya kwanza nitaimba nyimbo zangu live kwa kutumia bendi kuanzia wimbo wa Sawa, My Love, Tunapendana na nyingine nyingi,” alisema Mobeto.

 

Naye, Mr. Blue alizungumzia tamasha hilo, kuwa atafanya shoo ambayo itakuwa sapraiz kwa mashabiki wote watakaojitokeza.

 

“Shoo zangu mzee hazitabiriki. Nimejiandaa vya kutosha kwa hiyo niwaombe tu mashabiki wajitokeze kwa wingi kwani nitagonga ngoma baada ya ngoma. Njooni Dar Live tujimwageee,” alisema Mr. Blue.

 

Wakali hao walipata pia fursa ya kutembelea studio za +255 Global Radio na kuzungumza mengi waliyopania kuhusiana na tamasha hilo ambalo linawakutanisha kwa mara ya kwanza pamoja.

 

Katika tamasha hilo kiingilio kitakuwa ni Sh 5,000 tu, wasanii wengine watakaokuwepo ni Mr. Blue, Chidi Benz, Mzee wa Bwax na Easy Man.

Wakiwa ndani ya Studio za +255 Global Radio kwa mahojiano ya tamasha hilo.

Mobeto na Mr Blue kabla ya kufanyiwa mahojiano na +255 Global Radio.


Loading...

Toa comment