The House of Favourite Newspapers

Mobetto Ajuta Kuweka Picha Zake Chafu Mitandaoni – Video

IKIWA ni saa chache baada ya wafanyabiashara za mitindo na wasanii wa Bongo Movies, Hamissa Mobetto na Irene Uwoye kuwajibishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa makosa ya kuweka picha za nusu uchi mitandaoni kinyume na kanuni za maudhui mtandaoni za mwaka 2018, wasanii hao wamewaomba radhi mashabiki wao na kujutia kwa vitendo walivyofanya.

 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mobeto ameandika;

“Naomba radhi kwa umma: Husika na kichwa cha habari hapo juu, Mimi Hamisa Mobetto, ambaye ni mfanya biashara wa mitindo (fashion entrepreneur) hapa nchini Tanzania na pia ni raia wa Tanzania 🇹🇿 ninaomba kutumia fursa hii kuomba radhi kwa Watanzania na wengine wote ambao ni watumiaji wa mitandao kuhusiana na kitendo cha mimi na washabiki zangu (fans) wangu kutuma picha zangu zinazoonyesha nusu utupu kwenye page zao za Instagram.

 

“Pia natumia fursa hii kuwashukuru Kamati ya Maudhui kwa jinsi walivyoniita kwenye kamati yao na kunipa nafasi ya kujitetea na mwisho kufanya uamuzi wenye haki kwangu na kwa wapenzi (fans) wangu wote, ninawashukuru sana.🙏🏾

 

“Mwisho kabisa niwahusie vijana wenzangu kuepuka kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwani kwa sasa kuna sheria kali zinazokataza picha mbaya kutumwa kwenye mitandao .naomba pia wapenzi (fans) wangu kuanzia sasa kutuma picha zangu zenye staha au kutumia biashara zangu kunisapoti. Nawashakuru sana na mbarikiwe sana.❤🙏🏾

 

Hii imekuja baada ya TCRA kumpa onyo la mwisho msanii huyo kumtaka asirudie tena, endapo atakiuka maagizo hayo, atachukuliwa hatua kali za kisheria huku ikimtaka pia kuweka tangazo kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwaomba msamaha Watanzania na kuwataka kutosambaza picha zake za nusu uchi.

Comments are closed.