Mohamed Salah Achongewa Sanamu, Hafanani nayo, Inachekesha!

SANAMU za kuchekesha na zisizofanana na nyota wa soka ambazo zimekuwa zikichongwa, hivi karibuni zimefika kwa mwanasoka maarufu wa Misri,  Mohamed Salah, ambaye sanamu yake imewekwa katika ukumbi wa Mkutano wa Vijana Duniani unaofanyika huko  Sharm El Sheikh, Misri.

Sanamu hiyo imechongwa na raia wa Misri, Mai Abdel Allah ambaye huenda alizipatia sanamu kadhaa  alizochonga, lakini kwa sasa ukweli ni kwamba hii ya Salah, ameikosea sana.

Watu wamekuwa wakiifananisha sanamu hiyo na mwanamuziki wa Uingereza,  Leo Sayer!   Haifanani kabisa na ya Salah!

Hivyo, Salah amejiunga na nyota wa soka  kama Cristiano Ronaldo, Asamoah Gyan na Michael Essienwhose, ambao hawafanani kabisa na sanamu zao.

 

Toa comment