Mohammed Dewji ‘Mo’ Ameteua Kamati Ya Mashindano Simba
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba Sc, Mohammed Dewji ‘Mo’ ameteua Kamati ya Mashindano ya klabu hiyo ambayo itakuwa na wajumbe saba.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo Agosti 1, 2024 imebainisha Wajumbe hao walioteuliwa ambao ni Mohamed Nassor, Azan Said, Richard Mwalwiba, Nicky Magarinza, Juma Pinto, Farid Nahdi na Farouk Baghozah.