The House of Favourite Newspapers

MOHINI DEY: MSICHANA WA KIHINDI MPIGA GITAA LA BESI

Msichana wa Kihindi kutoka Mumbai, Mohini Dey.

JE, umewahi kumsikia, kumsoma au kumwona Mohini Dey, msichana wa Kihindi kutoka Mumbai ambaye ni mmoja wa wapiga magitaa ya besi mahiri duniani?

 

Binti huyo huliungurumisha gitaa hilo katika namna ya ajabu kama vile anacharaza gitaa la kawaida ambapo wapigaji hutembeza vidole kwa kasi.  Jarida la Forbes la India liliwahi kumpigia kura kama “mmoja wa vijana 30 walio chini ya umri wa miaka 30 wenye taathira kubwa zaidi nchini humo.”

 

Watu husema mtoto wa nyoka ni nyoka.  Mohini ambaye sasa ana umri wa miaka 18, ni binti wa mpiga gitaa la besi nchini humo, Sujoy Dey.  Kutokana na umahiri huo ambao ni dhahiri alirithishwa na baba yake huyo, ameweza kulikung’uta gitaa hilo akishirikiana vyema na wanamuziki mashuhuri duniani kama vile John McLaughling, A.R. Rahman,  Zakir Hussain, Steve Vai, Ranjit Barrot, George Brooks,  Babu Choudhary na wengineo.

 

Katika kukionyesha kipaji chake, Mohini aliunda kundi la muziki la Generation  na dada yake mdogo aitwaye Esani Dey ambaye naye ni mpiga gitaa, na mpiga ngoma mwanamme, Gino Banks.

Umahiri wa kipaji cha Mohini unadhihirishwa na pale mtu anapomsikia au kumwona katika video alizofanyia kazi yake hiyo.

WALUSANGA NDAKI  NA MITANDAO

Comments are closed.