The House of Favourite Newspapers

Molinga Achukua Ufalme Yanga

NYOTA Mkongo wa Yanga, David Molinga ameweka ufalme wake ndani ya klabu hiyo kwa siku za hivi karibuni kutokana na rekodi yake ya upachikaji mabao ambayo ni saba.

 

Molinga ambaye amesajiliwa msimu huu katika hatua za mwisho za dirisha la usajili, kwa sasa huenda akawa ndiye mshambuliaji moto ndani ya klabu hiyo kutokana na kasi yake ya kufunga.

 

Kasi ambayo alianza nayo winga, Mnyarwanda Patrick Sibomana kipindi cha maandalizi ilisababisha aonekane ndiye atakuwa tegemeo kwenye kufunga lakini kibao kimegeuka.

 

Katika mechi ambazo Molinga amecheza za kirafi ki pamoja na za Ligi kuu Bara amefunga jumla ya mabao saba mpaka sasa.

 

Straika huyo alifunga mabao hayo kwenye mechi za kirafi ki dhidi ya Toto Africans (3-0) alifunga mawili, Friends Rangers (4-2) mawili Pamba SC (1-1) bao moja pamoja na mechi ya ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania sare ya 3-3 akifunga mabao mawili.

 

Staa huyo kwa mara ya kwanza Oktoba 27, mwaka huu ndipo ataweza kutumika kwenye mechi za kimataifa ile ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids ya Misri, baada ya awali usajili wake kuwa na tatizo. Ikumbukwe mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Bara, Yanga imefunga mabao manne katika mechi tatu na Molinga akifunga mawili.

Comments are closed.