visa

Molinga Amtisha Kagere Bongo

KASI ya kufunga mabao aliyonayo David Molinga wa Yanga, kwa namna moja ama nyingine inamtisha Meddie Kagere wa Simba.

 

Kagere anaongoza kwa mabao akiwa nayo 12, amemuacha Molinga kwa mabao matano. Molinga ana saba.

Hivi karibuni, Molinga alifunga mabao matatu katika mechi tano zilizopita za Yanga na kumfanya kuibuka kwa kasi.

Wakati Molinga akifunga, Kagere amesimama kidogo kwani mara ya mwisho kufunga bao ilikuwa Januari 29, 2020.

Rekodi zinaonyesha kuwa, wakati Kagere ana mabao 11, Molinga alikuwa nayo manne. Tofauti ilikuwa mabao saba, lakini kwa sasa tofauti ni tano.

 

Awali wakati Molinga anatua Yanga akisajiliwa na Mwinyi Zahera aliyekuwa akiinoa timu hiyo kabla ya kutimuliwa, alisema Molinga atamaliza msimu huu na mabao si chini ya 15.
Toa comment